Aina: Kimani wa Mbogo

Kimani wa Mbogo, anayejulikana kwa lakabu Mwanagenzi Mtafiti ni mtunzi wa mashairi nchini Kenya. Baadhi ya mashairi yake yamefanyiwa uchambuzi na kuzua mijadala redioni. Mengine yameghaniwa na magwiji wanaojulikana kwa kughani, akiwemo Abdallah Mwasimba (KBC). Majarida na magazeti mbalimbali (likiwemo Taifa Leo) pia yamechapisha mashairi yake kwa muda mrefu tangu mwaka wa 2005.