Kwangu Huwa Maridhia

Mapenzi ni jambo la mtu na hiari yake. Hulazimishwi kumpenda huyu ama yule. Wengine watakuvunja moyo na kukwambia unayempenda si mwema. Kila mtu ana ila zake. Hakuna mwanadamu aliye kamili asilimia mia moja. Unapozitambua ila za mke wangu, jua na usinipashe kwa kuwa nilizijua kitambo. Wengine watakupasha mengi yasiyo na maana wala ukweli kuhusu mpenzi wako ili umwache amtongoze. Mara nyingi udaku hupotosha na kuangamiza wawili wapendanao ama hata familia.

Shairi lifuatalo la tarbia lina mengi ya kufahamisha. “Sijali mnavyomwita, kwangu huwa maridhia”. Hata mseme, mmbadike majina ama mmdharau, kwangu nampenda tu. Mpenzi wa mtu ni mpenzi wake tu yawache ya kwao huyawezi. Hebu lisome na utafari kwa kina. Ufurahiae uhondo wa shairi hili la Kimani wa Mbogo analoliita “Kwangu huwa maridhia”. Kwangu Huwa Maridhia