Aina: Ukaraguni

Ukaraguni ni shairi ambalo vina vyake vya kati na vya mwisho hubadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

Wachinjaji

Wachinjaji

Niliamuwa kutunga shairi hili, baada ya kupiga tathimini hapa katika visiwa vyetu vya Zanzibar watu wengi au niseme wote ambao hujishughulisha na kazi za uchinjaji wa wanyama, wanafanya shughuli hizo nyakati za usiku wa manane au karibu na alfajiri.

Kilichonishangaza na kuniduwaza na hadi kuamua kushika kalamu na kuandika shairi hili kwa nini wasubiri kufanya kazi hiyo usiku? ilhali mchana kuna mwangaza wa kutosha wakati usiku wanahitaji taa ili kufanya kazi yao hio, pia endapo usiku ikitokea mnyama ametoroka si rahisi kumkimbiza na kumkamata kwa sababu ya kiza cha usiku, lakini kama wangalifanya kazi hio muda wa mchana ingekuwa ni rahisi kumkamata mnyama endapo angejaribu kutoroka.

Lakini yote kwa yote, kazi ya fasihi ni uwanja mpana, shairi hili licha ya kuwalenga washairi bado linatoa nafasi pana zaidi kwa wanafasihi kuangalia mambo mengine ambayo yanapenda kufanywa usiku ilhali endapo jambo lile lingefanyanywa mchana basi pia ingekuwa ni aula na lingeepusha gharama za ziada ambazo labda usiku zingehitajika ngarama hizo.

Read More Wachinjaji