Historia ya Ushairi

Ni vigumu sana kuelezea wakati ushairi wa Kiswahili ulipoanza. Wapo baadhi ya watu wanoamini kuwa ushairi ulikuwepo tangu Karne Pili. Wapo pia wanaoamini kuwa ushairi ulianza mtu alipobuni lugha. Lakini inaaminika kuwa, chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni kutokana na nyimbo zilizotumia nyakati za sherehe mbalimbali kama harusi, jando, nyakati za kufanya kazi, nk. Nyimbo hizo hazikufuata arudhi tunazozifahamu za ushairi wa kisasa, ila baadaye ziwekwa vina na hatimaye kuwiana hata kwa mizani.

Zipo nadharia nyingi zinazoelezea kuhusu historia ya Ushairi tangu wakati huo hadi sasa. Ipo nadharia inayodai kuwa Chimbuko la ushairi wa Kiswahili ulitokana na ujio wa Waarabu. Nadharia nyingine inasema kuwa Chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni kwa jamii ya waswahili wenyewe. Lakini ni dhahiri kwamba chimbuko la Ushairi wa Kiswahili ni kutoka kwa Waswahili wenyewe. Waswahili wana utamaduni wao ambao ulikuwepo hata kabla ya ujio wa Waarabu. Na waliutumia Ushairi huo katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Historia ya Ushairi wa Kiswahili ni ndefu mno ila wataalamu wameumegawanya muda huo wote kwa vipindi vinne.

Kipindi Cha Kwanza (Urasimi Mkongwe)

Kipindi hiki ni wakati wa mashairi yaliyotungwa kabla ya karne ya kumi na nane. Katika kipindi hiki, mashairi yalikuwa kakitungwa ila hayakuwa na utaratibu wa vina, vina, mizani na beti kama ilivyo katika mashairi ya kisasa. Mashairi ya siku hizo yalikuwa kama nyimbo tu na yalikuwa na mishororo mirefu. Mashairi hayo yalibadilika kimaudhui, jamii nazo zikipambana kutunga kwa maudhui mbalimbali.

Mashairi ya myakazi hizo, yalipashwa tu wakati wa sherehe mbalimbali kwa kuwa ustaarabu wa kuandika ulikuwa bado kwa Waswahili. Mabadiliko mengi yalifanyika Waarabu walipofika pwani ya Afrika Mashariki. Waarabu walikuwa na mashairi yao yaliyokuwa na vina beti, mizani na maudhui ya kidini (dini ya Kiislamu). Tangu wakati huo, mashairi yakfuata mkondo huo. Waswahili wakafunzwa hati ya Kiarabu ili kusoma Kurani Tukufu.

Hizo ndizo nyakati ambazo inadhaniwa kuwa shairi la kwanza liliandikwa kwa kufuata kanuni za Ushairi. Japo kulikuwa na mashairi mengine hapo awali, Utenzi wa Tambuka (Chuo cha Herekali) unadaiwa kuwa wa kwanza kuandikwa kwa kufuata kanuni za Ushairi. Utenzi huo ulitungwa na Mwengo Bin Athumani (1728-1840) na ulihusu maisha ya Sultani wa Pate ‘Fumo Laiti Nabhani’.

Tungo nyingine za wakati huo:

 1. Utenzi wa Hamziya (1749) – Sayyid Abdarus
 2. Utenzi wa Mwanakupona (1859)
 3. Utenzi wa Al-Inkishafi (1813) – Sayyid Abdallah A. Nassir
 4. Utenzi wa Rasi-al-Ghuli
 5. Utenzi wa Shufaka
 6. Tungo za Muyaka bin Haji Al Ghassany (1776-1840)
 7. Tungo za Ali Kofi
 8. Tungo za Bwana Mataka
Kipindi Cha Pili (Kipindi cha Utasa)

Kipindi hiki ni miaka kati ya 1885 na 1945. Huu ulikuwa wakati wa utasa. Huu ulikuwa wakati wa ukoloni. Mashairi mengi yaliyotungwa katika kipindi hiki yalihusu utumwa na kujikomboa kutoka kwa wakoloni.

Baadhi ya waliotunga katika kipindi hiki ni kama:

 1. Utenzi wa Vita vya Majimaji
 2. Utenzi wa Abdirahman na Sufiyani (1939-1945) – Hemed Abdalla
Kipindi Cha Tatu (Urasmi Mpya)

Kipindi hiki kilikuwa kati ya 1945 na 1960. Washairi walitunga kwa kufuata kanuni za ushairi. Wengi wa watunzi hao walitunga mashairi ya tarbia ingawa wengine kama Shaana Roberts walitunga aina tofauti ya mashairi. Kipindi hiki kilikuwa cha Wanajadi au Wanamapokeo walishindania ufundi. Ilikuwa ni lazima kila mtunzi kutumia arudhi za ushairi ili kuonyesha kuwa, alikuwa bora kuliko mwengine. Shairi ambalo halikufuata kanuni hizo, halikuaminika kama shairi kamili na liliitwa guni. Waliamini kuwa shairi ni lazima liwe urari wa vina na ulingasnifu wa mizani.

Tamasha mbalimbali ziliandaliwa na watunzi kuwasilisha tungo zao na kufanyiwa uamuzi na watunzi waliobobea wakajulikana kama mashekhe. Waliofaulu walivikwa umalenga nawaliopungukiwa katika arudhi yoyote kubezwa na kuvikwa guni.

Watunzi waliosifika sana wakati huo walikuwa kama:

 1. Mwengo Bin Athumani
 2. Muyaka bin Haji
 3. Mwalimu Sikujua
 4. Said Karama
 5. Amri Abedi
 6. Ahmad Nassir
 7. Shaaban Robert

Umaarufu wa washairi wa kipindi hiki ulidhihirika wakati wa tamasha mbalimbali na sherehe kama za arusi, mazishi na burudani. Tamasha hizo zilisaidia kunoa na kuboresha vipawa vyao.

Kipindi Cha Tatu (Urasmi Mpya)

Katika kipindi hiki, kulizuka wasomi wenye ujuzi katika Fasihi ya Kiswahili. Wasomi hao walijiita Wanamapinduzi. Walijitokeza na aina ya mashairi yanayojulikana kama Mashairi Huru na kudai kuwa yanakubalika katika kama mashairi mengineyo.

Wanamapinduzi hao walisitiza kuwa mashairi ya arudhi yalimfunga sana mshairi kupasha ujumbe wake vizuri. Walidai kuwa mshairi hakuweza kujieleza vizuri kwa kuwa ilikuwa ni lazima ajibiidishe kwanza kutafuta maneno yatakayolinganisha vina na kutosheleza mizani. Waliamini kuwa mtunzi ana uhuru wa kutunga aina za mashairi wazipendazo bora tu wapashe ujumbe kwa hadhira. Washairi hao walitunga mashairi bila kujali arudhi za ushairi, jambo ambalo lilizua mgogoro katika Ushairi wa Kiswahili.

Baadhi ya watunzi hao ni kama:

 1. Euphase Kezilahabi
 2. Mugyabuso Mulokozi
 3. Ebrahim Hussein
 4. Alamin Mazrui
 5. Kithaka wa Mberia
 6. Kulikoyela Kahigi