Balagha

Balagha ni mbinu ya kuuliza swali lisilohitaji kujibiwa. Anayeuliza huwa na nia ya kuchochea msikilizaji ili afuate mkondo wake wa fikira.Katika shairi “Unani sogora?”, mtunzi ametumia mbinu ya balagha. Amekasirishwa na sogora anayefanya kazi yake usiku na kuuwafanya watu wasilale. Anapouliza ‘U nani sogora?” hahitaji wala kutarajia jibu. Hili ni swali la balagha.

Mfano: Unani Sogora

Wadunda zinavuma, ufundi unao,
Hukosi adhama, fundi wa mwambao,
Ungetwanga ngoma, muda ufaao,
Unani ewe sogora, kucha tusilale?