Kinaya

Hii ni mbinu ya kutoa maelezo ya kitu au hali iliyo kinyume na matarajio.Ubeti ufuatao umenukuliwa kutoka kwa shairi linalojulikana kama “Jina langu libomoe”. Tunavyojua ni kuwa Jehanamu kutakuwa tu na adhabu. Hata hivyo, kutumia hili shairi mtunzi anaonysha kuwa mtu anayemharibia jina atalipwa huko.

Mfano: Jina langu libomoe

Mshahara mwingi sana, usubiri utapewa,
Mwishowe utauona, ujira kukabidhiwa,
Sikia ninalonena, sitaki kukashifiwa,
Jina langu libomoe, Jehanamu utalipwa!