Ndege si ndege tu. Rangi tofauti zake huwa ishara ya jambo fulani. La muhimu kuelewa ni kwamba ndege mweupe huwa ishara ya amani! Ndege Mweupe


Ndege Mweupe

Huko kwingine kwawaka, damu ingali kondeni,
Vilio vinasikika, hakukaliki jimboni,
Huzuni imetufika, kila kutwa kaburini,
Tumeni ndege mweupe, mwekundu ana majanga.

Hata muweke lawama, Mungu ndiye ataweza,
Huyo ndiye wa rehema, baya likijitokeza,
Huyatenda yalo mema, bila yeyote kubeza,
Tumeni ndege mweupe, mwekundu ana majanga.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*