Marko John Kinyafu

Marko John Kinyafu alizaliwa Juni 22 mwaka wa 1995 22 mjini Dar-es-salaam,Tanzania. Ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto watatu. Lakabu yake Muumini wa Kweli ndilo jina alitumialo katika kazi zake za sanaa za maigizo ya jukwaani na kazi za ushairi.

Marko alianza shule ya awali mwaka 2001. Alisoma kwa miaka miwili na mwaka 2003 alianza shule ya msingi Kitunda iliyopo Ilala vijijini. Alisoma hapo mpaka darasa la saba na mnamo mwaka 2009, akamaliza elimu yake ya msingi, ndipo akafulu mitihani yake ya elimu ya msingi na kuchaguliwa kujiunga na shule ya sekondari Kivule iliyopo Ilala vijijini jijini Dar es salaam.

Alisoma hapo Kivule kwa miaka yote minne kwa masomo ya biashara na mwaka 2013 alifanikiwa kumaliza elimu yake ya sekondari. Anamshukuru Mwenyezi Mungu aliyemsaidia kufaulu na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondari ya Benjamini William Mkapa iliyopo Kariakoo barabara ya Uhuru jijini Dar es salaam. Hapo Alisoma mchepuo wa Historia, Gografia na Uchumi (HGE 2014-2016) na hatimae alifanikiwa kumaliza masomo yake na kufaulu vizuri. Mwezi Octoba mwaka 2016 alianza masomo ya shahada ya kwanza. Kwa sasa nipo anatafuta shahada ya kwanza ya Bima na Usimamizi wa Majanga katika chuo cha Usimamizi wa Fedha kilichopo Posta Jijini Dar es salaam.

Mwaka 2007 ndipo nilipoanza kuishi maisha ya sanaa wakati tukiwa tunafanya maigizo na ushairi katika shule ya jumapili ya KKKT Kitunda Kuu, lakini siku zilivyozidi kwenda nilikuwa nikiona shauku ya kuishi katika maisha ya sanaa ikizidi na ndipo mwaka 2012 niliamua kuanza
kujaribu kuandika mashairi na kiu yangu ilikuwa ni siku moja nije kuona na kusikia mashairi yangu yakiimbwa sehemu mbalimbali.

Japo ni kweli alianza kwa ugumu kwa asababu hakuwa na mbinu zozote za utungaji, siku zilivyozidi kwenda ndipo alizidi kukua japo ni kwa mwendo wa kobe. Baada ya kumaliza kidato cha sita sasa aliamua kuanza upya kwa mwendo wa farasi. Alianza kufanya utafiti juu ya ushairi na kusoma kazi za washairi wakubwa kama Mzee Haji Gora Haji ,Shaabani Robert na chambuzi za Profesa Mlokozi juu ya fani ya ushairi.

Marko anamshukuru Mungu kwamba jitihada zake zilizaa matunda na akaweza kuandika mashairi mengi na michezo ya kuigiza na hadi sasa anaendelea na kazi yake ya utunzi wa maigizo na mashairi. Pia anaandaa vitabu viwili, kimoja kikiwa kinaelezea maisha yake ya ushindi na kingine kikiwa ni diwani ya ushairi.

Marko ameitwa kwenye mahojiano mbalimbali na vituo vya habari kuhojiwa kuhusu maisha yake ya sanaa. Huu ni ushaidi tosha kuwa Mungu anazidi kumwezesha. Sababu ya kujiita Muumini wa Kweli  alitaka kuwafahamisha watu wanaodhani kuwa mtu yeyote anaefanya kazi za usanii ni muhuni lakini si kweli.

Yeye binafsi anafanya kazi za ushairi na maigizo sehemu yoyote anapohitajika lakini bado msingi wa imani yake aliofunzwa bado anaushika na kuuishi ndio maana akasema angetaka watu waelewe kuwa yeye ni Muumini wa kweli. Awape rai washairi wachanga wasikate tamaa kwani palipo na juhudi na nia ya kweli basi mafanikio yapo zaidi. Muhimu ni kuweka subira na kumtegemea Mungu.