Mwangi wa Githinji

Mwangi wa Githinji ni mshairi ambaye amekuwa akiyatunga mashairi kwa miaka mingi. Ni Mwalimu katika shule ya msingi Limuru Township. Amekuwa akitunga mashairi ya sherehe za kifamilia pamoja na sherehe za mahasibu wake. Mashairi yake yameweza kutumika katika tamasha za mziki hadi kiwango cha kitaifa. Mashairi yake huacha wengi wakibung’aa kwa tungo zenye kuelimisha si haba. Mwangi wa Githinji yu hatuani kuandaa diwani (Sikate Tamaa) ambayokwa sasa ndipo inakamilika. Amewahi kufunza shule ya Taramia ya Kanini York Murang’a mwaka 2012-2014 na shule ya Msingi Gaicangere murang’a mwaka 2015-2016.

Mwangi wa Githinji alizaliwa mwaka wa 1989 Disemba 28. Ni wapili kuzaliwa katika familia yake. Ana dada wawili na kaka mmoja. Wazazi wake ni walezi wasiomithilika walivyomlea katika Ukristo. Katika tungo zake anapenda kuwapa sifa jinsi walivyomfunza kukemea uzembe. Ni wenye bidii za mchwa wanaoenda kuhemera.

Mwangi alizaliwa katika kaunti ya Nyeri , Othaya, wadi ya Karima karibu na kwao rais mstaafu Mwai kibaki. Mwangi almaarufu Malenga wa Mchanga Kati alijipa lakabu hiyo kwa sababu kadhaa;

  1. Wazazi wake walimlea katika Maisha ya ‘kina pangu pakavu tilia mchuzi’. Wazazi wake walitegemea mchanga kwa ukuzaji wa kahawa na maboga angaa wapate cha kutia mdomoni. Anaamini watu hawapendi kufanya kazi ya ‘mchanga’ vile wanadai ni uchafu. Mchanga walioudharau ndio uti wa mgongo wa Maisha ya kila mlimwengu. Mchangani mbegu hupandwa ikamea, inakuwa mche na baadaye mmea unaonoga au mti mkubwa wenye manufaa kwa mwanadamu.
  2. Alijiita malenga wa mchanga Kati kwa vile amezaliwa kwenye pande za mlima Kenya na safu ya milima Nyandarua mkoa wa Kati. Anaamini ni sehemu zisizo na watu wanaokienzi Kiswahili, hivyo anajitambua kati ya Waswahili wachache wa mkoa wa kati. Hamasisho kwa watu wa kwao ni kuwa sio lazima kitovu kikatiwe katika maeneo ya mwambao ndipo uwe malenga anayetajika. Popote, lolote lawezekana.

Mwangi wa Githinji amesomea chuo cha walimu cha Tambach Eldoret. Alitaabika kupata karo na hata fulusi za masurufu na kwa hivyo akawa anatafuta vibarua vya hapa na pale wakati wa likizo. Alijiunga na chuo cha walimu mwaka wa 2010 na kuhafili mwaka wa 2012. Chuoni alichimbua Vito vya Uswahili kwa kishindo na kutunga mamia ya mashairi. Hata hivyo, hakufaulu kuyachapisha magazetini kwa vile yaligugunwa na panya alipokuwa ameyahifadhi. Akabaki kula mwande kuyachapisha lakini hakuwa mwendanguu. Laonekana jambo la utani ila hilo ni jambo moja kati ya dhiki zilizoweza kumpata katika bahari ya ushairi. Mashairi yake yalikwisha gushiwa wakati mmoja na wengine ila hakufa moyo asi. Kama shairi moja lake la kikai alivyotunga ‘usife moyo’.

Mwangi alijiunga na shule ya upili ya Giakanja 2006-2006. Shuleni alijulikana kama Mzee Kamusi vile aliandamana na kamusi kama Bwana Shamoo na kijibwa chake. Katika kidato cha pili alinunua diwani yake Boukheti Amana almaarufu malenga wa vumba (Sikate Tamaa) alipoweza kujifunza mengi.

Mwangi alikuwa shabiki wa kipindi cha Kamusi ya Changamka kilichoanzishwa na Nuhu Zubeil Bakari. Isitoshe yeye ni mwanagenzi katika kipindi cha Nuru ya lugha kinachopeperushwa naye Hassan mwana wa Ali pamoja na wenzake. Walla bin Walla pia ni Mwalimu wake kwenye vipindi mbalimbali anapohojiwa. Kupitia mitandao ameweza kuwa akichangia kwenye mashairi ya wanaochipuka. Atangaye sana najua hujua. Anawapa kongole za dhati washairi kama Kimani Wa Mbogo, Victor Mulama, Mwinyi Bokoko na wengine. Katika nchi jirani ya Tanzania anawapongeza akiwemo dada Sharifa Mohamed, Husein Kipanga Mtoa, na mashairi ya Rangi Moto.

Mwangi wa Githinji alinzia safari ya masomo katika shule ya msingi ya Karima Othaya mwaka wa 1997 hadi mwaka wa 2005 alipofanya mtihani wa kitaifa. Mwalimu wake wa nyakati hizo Bw. Maina Wanyiri amechangia pakubwa kumlea katika bahari ya ushairi.

Wosia wake kwa watunzi wanaochipuka ni kuwa; kuuliza si ujinga, kutouliza ndio ujinga. Anaamini lugha ni kufunzana wala si kufukuzana na kuchekana. Cha msingi ni kufanya utafiti na kwenda na wakati. Wajue bahari ya ushairi inazidi kukua. Ya awali maswala yalikuwa tofauti na yanayoibuka leo. Utungapo shairi piga alinacha kama lina funzo kwa ulimwengu wa kisasa. Jinsi Maisha yanavyobadilika nawe kama mshairi ubadilike. Hata hivyo sisemi tungo za kale tuzipuzilie asi. La hasha, tukumbuke ngoma ya vijana haikeshi.

Ni vyema kurejelea tungo za malenga wa hapo awali ili tusipotoke kiarudhi za mashairi. Tusitumie mashairi kuwadhalilisha wengine ila yawe ya kusifu la kusifika au kukashifu la kukashifika.

Mwangi wa Githinji ni Mwalimu mcheshi ambapo kila wakati anapoongea kwa lugha utadhani anaboboja maneno ila utaachwa ukishangaa kuelewa maana. Malenga wa Mchanga Kati ni mraibu wa kusoma vitabu vya hadithi, kutazama sinema, kusikiza mziki wa taarabu, kuandika hadithi fupi na riwaya. Ni matumaini yake kuwa kwa miaka ya usoni kazi nyingi zake zitakuwa zimeharirishwa na hata kuchapichwa kwa minajili ya kufunza jamii na mataifa.

Heri kufa macho, liko kufa moyo,
Ziko dhiki kocho, za nyonga kijoyo,
Winamisha macho, vipeni hunayo,
Usife na moyo.

Walala walia, amani hunayo,
Mate walala, poneo hunayo,
Chawa kukulia, na ngeu hunayo,
Usife na moyo.

Baridi shadidi, yaganda mwiliyo,
Kutinga yabidi, ya dunda rohoyo,
Yakwamusha radi, kupapa moyoyo,
Usife moyo.

Kibanda wushipo, kweli kidogoyo,
Nacho cha mkopo, moja elufuyo,
Dirisha halipo, we ndo wajuayo,
Usife moyo.

Ukivaa vazi, yote mararuyo,
Sokisi si jozi, hazifananiyo,
Huna hata jezi, ila tu wombayo,
Usife moyo