Wafrika Twajivunia

Nakumbuka enzi zile, tuliishi kwa amani,
Na masomo ya kikale, tulisoma kitamani,
Ngao yetu na mishale, tulishinda na vitani,
Miungu wetu wa kale, tulizidi waombani,
Mila zetu zilezile, tulipenda kiundani,
Wazungu situtusini, twavunia uafrika.

Na wivu lituonea, kwa madhari yetu safi,
Mkazidi tuchomea, eti sisi wasafi,
Tuliwapa historia, mkakana kwa ulafi,
Iwaje lituhurumia, kutuzaba kwayo kofi?
Tena litukemea, mila zetu zilo safi,
Wazungu situtusini, twavunia uafrika.

Litujia kirafiki, kwalo neno lake Mungu,
Mkasema kuhakiki, tuwachane na miungu,
Kumbe hamtutaki, kutufanya si wazungu,
Na utwumwa lishiriki, kotekote ulimwengu,
Wengi wetu lifariki, kipitia malimwengu,
Wazungu situtusini, twavunia uafrika.

Mabeberu kiwasili, linyakuwa yetu shamba,
Tukisea na asili, ushuru mlituomba,
Mila zetu za asili, lirarua kama pamba,
Lituchosha yetu mili, kwa makali yake simba,
Mateso litukabili, tukawa roho ya mamba,
Wazungu situtusini, twavunia uafrika.

Mlidhani sisi duni, mbona mkaja kwetu?
Mlitaka yetu madini, mlikosa kweli utu
Kutuwacha masikini, kuchukuws kila kitu,
Mlijawa matamani, kumuua kila mtu,
Namuita nyie wahuni, mtakayo mili yetu,
Wazungu situtusini, twavinia uafrika.

Haki yetu iko wapi, kama sisi binadamu?
Japo muda ni mfupi, nauliza kufahamu,
Watu wetu wako wapi, lipoteza kwayo damu?
Mezindua njia ipi, na suluhu la kudumu?
Tatulipa kweli vipi, ama sisi wahukumu,
Wazungu situtusini,twavunia uafrika.

Muda wangu wayoyoma, sitopita kamwe hapa,
Yangu yote nimesema, nabandua mali papa,
Wazungu sije tusema, na la rongo kutoapa,
Mila zetu tutotema, ninakiri bila pupa,
Afrika wetu mama, na kwingineko ni papa,
Wazungu situtusini, twavunia uafrika.

© Brian Mutambo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *