Afande Hongo Sitoi

Darahimu sitotupa, ufisadi siingiwi,
Kaziyo sitokulipa, usipolipwa hupowi,
Usipopewa watapa, haki zanguhuelewi,
Afande hongo sitowi, ufisadi naogopa!

Darahimu sendi kopa, ofisaa sipagawi,
Ufisadi nitahepa, hela haziniokowi,
Kwa lake Mola naapa, zangu fedha haziliwi,
Afande rushwa sitowi, ufisadi naogopa!

Siingii yako kwapa, mroho dafu hufuwi,
Ujaribu kujikwepa, ofisaa hutombowi,
Ujifanye unanyapa, wadhanihutambuliwi,
Afande hongo sitowi, ufisadi naogopa!

Kisheria wajichapa, kwa furahahuchachawi,
Mtima utakupapa, usemapo sifichuwi,
Kifisadi kunenepa, neema hupanukiwi,
Afande chai sitowi, ufisadi naogopa!

Mmeo moyo wajipa, hakunalohutendewi,
Usidhani nitakupa, rahisi silaghaiwi,
Ilani yangu nakupa, ufisadi sifanyiwi,
Afande hongo sitowi, ufisadi naogopa!

© Kimani wa Mbogo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *