Katika nyakati za ukoloni wengi waliteseka na kupoteza mali yao. Wakoloni hawakujali lolote au yeyote. Walitekeleza tendo lao la kuwanyanyasa Waafrika na kuwatumia tu kama chombo ili kujinufaisha. Mjoli Mtukutu


Mjoli Mtukutu

Ni mjoli mtukutu, kwa waulizao nani,
Kitinda mimba mwanetu, mzawa wa ukoloni,
Aliliaye baretu, lilondoka utumwani,
Ni mjoli mtukutu, mzawa wa ukoloni.

Mabazazi waso wetu, uhuru walotuhini,
Tangu lini kawa kwetu, ukupe hatuuoni,
Walotupiga kitutu, waishi kwetu barabi,
Ni mjoli mtukutu, mzawa wa ukoloni.

Sikufiti utukutu, kwao wanaugenini,
Hufuata yalo yetu, ukweli ndo siwahini,
Nitatenda yalo utu, sifanyi ya ukoloni,
Ni mjoli mtukutu, mzawa wa ukoloni.

Haku situlii katu, watakavyo weupeni,
Sifwati lisilo letu, watakavyo weupeni,
Wasojua utukutu, waniitao mtini,
Ni mjoli mtukutu, mzawa wa ukoloni.

Usumbu wa mtukutu, mpenda utamaduni,
Apendaye yalo yetu, achukiaye wanuni,
Alipendalo baretu, lisokuwa utumwani,
Ni mjoli mtukutu, mzawa wa ukoloni.

Sifwati lisilo letu, watakavyo weupni,
Mabazazi waso wetu, ukweli ndo siwahini,
Sitendi lisilo letu, sifuati la ugeni,
Ni mjoli mtukutu, mzawa wa ukoloni.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*