Lisemwalo lipo na kama halipo laja. Ni methali ya Kiswahili inayotambulika sana. Soma hili shairi linaloelezea mengi kuhusu ukweli huu. Lisemwalo Lipo


Lisemwalo Lipo

Likinenwa lisikize, ulitie tafakuri,
Akilini liangaze, mdokezee Kahari
Kwanza usilitangaze, hivyo itakuwa heri,
Lisemwalo ndilo lipo, lisipokuwapo laja.

Ijue asili yake, tendo usiharakishe,
Msingi wake lifike, ndivyo ujishughulishe,
usingoje litendeke, hilo ulisuluhishe,
Lisemwalo ndilo lipo, lisipokuwapo laja.

Usipuuze waneni, hata wawe ni wazimu,
Usione ni utani, mawazo yakulazimu,
Lifikiri kwa makini, asaa kitu adhimu,
Lisemwalo ndilo lipo, lisipokuwapo laja.

Tafakaria uneni, uielewe maana,
Cha muhimu ni amani, jamii tukaungana,
Mambo usiyoamini, henda yakakufana,
Lisemwalo ndilo lipo, lisipokuwapo laja.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*