Si jambo la busara kunidharau. Hujui kesho au hatima yangu. Usinidharau! Usinibeze! Usinidhulumu! Mbona Wanizaba Kofi


Mbona Wanizaba Kofi

Kofi wanizaba, ndugu watakani?
Wako ni ujuba, uletao shani,
Kejeli si haba, kuwa sina peni,
Sina hata shaba, wanizabiani?

Mie nikipita, waniona pite,
Ewe waniketa, haki nisipate,
Daima nateta, kudondokwa ute,
Daima matata, kwako nisipite.

Dinari ndo sina, ndo wanidharau,
Katu sitakana, sijapata dau,
Nimeshakumbana, na nyingi dharau,
Bado sijaona, mwema angalau.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*