Ngonjera: Raia na Viongozi

Raia:
Amani …twalilia amani,
Twashidwa tufanyeje maovu kukithiri
Twawakimbilia viongozi twaomba mtusikie
Nyinyi ndio wokozi wetu…

Viongozi:
Nini ambacho sisi hatujamtendea
Kila mara mmejawa na lawama
Mkatuchagua sisi viongozi wenu
Lakini tutendacho shukrani hamna
Mnataka nini?

Raia:
Mwasema mmetutendea jambo
Lakini swali labaki….jambo gani hilo?!
Kila mara twahangaika..
Utulivu sisi hatuna kamwe..
Woga maishani kila uchao….
Aushi gani hii kuishi?!

Viongozi
Tegeni masikio yenu vyema…
Kama hamyaoni mazuri tuliyotenda na tunayozidi kutenda..
Twawaachia kazi…kazi sasa ni kwenu
Jifanyieni mtakalo…usumbufu hatutaki

Raia:
Ole wetu….viongozi pia wataka kutugeuka
Tulifanya makosa kuwachagua?
Tegemeo letu sasa ni gani
Twahitaji msaada kwa kweli..
Amani tuipate..

Kiangalia usalama…shida imekithiri.
Hatari barabarani tunawapoteza wapendwa wetu…nn kinachofanywa?!
Kiangalia somalia..utata mwingi..amani hakuna!!
Miaka mitatu nyuma twawapoteza wakufunzi katika shule kikuu…nn kilichotendwa..?
Jamani twazidi kuumia …tutafanyeje?!

Viongozi.
Kwa kweli mmenena yanayogusa mioyo
Usalama nchini hakuna..
Kiangalia ajali na vitisho zinazoripotiwa kila uchao
Twawaombeni msamaha
Sisi kama viongozi tumekosa
Twadhani tumetenda mema ila kunayo mengi hatujatenda….twawawia radhi

Raia.
Ni jambo jema kusikia..
Kama wasemavyo

© Cate Gatwiri

Maoni 3

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *