Mja Shukuru Mungu

Mwenza unayo bahati,uwache mingi mikogo,
Usililie kiatu,tazama ‘aso’ miguu,
Shukuru kwa upatacho, kikosa basi futuru.

Wazama anazo ngano, waleo mengi majabu,
Simba anayo makucha, naye ndovu na mkonga,
Nyani anao mkundu, binadamu kwa akili.

Msiri tembea kote, maongofu uyashike,
Mambo mawi achilia, sikutie matatani,
Mchele sema mtamu, mapishi yategemea.

Wa kukutenda mtende, aso tenda usitende,
Maisha ni kuyaishi, yaishayo si maisha,
Kukufa kama kondoo, ndiko kufa kiungwana.

Fimbo ya kwako mnyonge, anayelipa ni Mungu
Shukuru Mungu kwa yote, kwa yote shukuru Mungu.

© Mwangi wa Githinji

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *