Tikiti Maji

Nawaita ikhiwani, kitaka muwe majaji,
Sikiza nielezeni, utamu wangu mlaji,
Lipo hapa kiganjani, li tamu kama kileji,
Napenda tikitimaji, tunda bora shinda zote.

Tikiti huwa kijani, tena iliyo kolea,
Pindi ukatapo ndani, ni nyekundu watambua,
Ni rangi hazilingani, wekundu kijani pia
Napenda tikitimaji, tunda bora shinda zote.

Hapa Kenya pia yapo, zakuziwa ukambani,
Hayataki pa upepo, yaotapo ardhini,
Kila mara uvumapo, tunda huchanganyikani,
Napenda tikitimaji, tunda bora shinda zote.

Wapo wengi matikiti, kijani tena wekundu,
Tena wengi si katiti, kitale lama makindu,
Naomba tujizatiti, tuuwache u utundu,
Napenda tikitimaji, tunda bora shinda zote.

© Moses Chesire
(Sumu ya waridi) Kitale mjini

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *