Hashuo Lake

Kanisa nyumba ya Bwana, na ndio yetu makao,
Yetu mambi kwa Rabana, hayo kwetu huwa ngao,
Lolote kwa Maulana, kwetu huwa ni mazao,
Tutunze hashuo lake, nasi baraka tupate.

Kanisa si lazi’ jumba, yetu mwiyo ni sanika
Tumwombeapo Muumba, kwetu iwe ni baraka
Tufanyapo ya kuimba, burudani kwa Rabuka
Tutunze hashuo lake, nasi baraka tupate.

Moja kwetu ni kanisa, bali wengi waumini,
Walio zao laasa, pokelewa hekaluni
Vyema kanisa rembesa, jukumu letu kwa dini,
Tutunze hashuo lake, nasi baraka tupate

Kanisa na msikiti, hivi vitu ni vimoja,
Ndogondogo tofauti, lengo kwetu huwa moja,
Tunampenda kwa dhati, aliyewaumba waja,
Tutunze hashuo lake, nasi baraka tupate.

Mwisho mwisho nafikaa, kwetu si himizo hasi
Ila vyema kunyakua, nema hizi tuzihisi
Tuminipo kanisaa,kwa Mola ndilo kasisi
Tulitunze hashuo lake, nasi baraka tupate.

© Vincent Okwetso

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *