Jicho Langu

Kwa nini kuniadhibu, kwa hili langu jicho,
Ewe unipe sababu, sababu zilizo kocho,
Nieleze kwa kitabu, nisome kwa yangu macho.

Nikipitia karibu, penye mti wa matunda,
Maozi yanajaribu, kutazama, kuyatunda,
Na kumbe ni kuharibu, na sio kwangu kupenda.

Kipitia mitaani,mitaa yenye maduka,
Kwangalia dirishani, kutamania bazoka,
Hii kazi ya machoni, yanifanyia kuchoka.

Akipita mwanamke, ama iwe mwanamme,
Yanibidi niteseke, kwao wote nitazame,
Lafanya nitatizike, jicho lafanya nizame.

Ukasoma bibilia, hata korani tukufu,
Zinakufafanulia, jichoni Pana udufu,
Na maovu angalia,uisome misahafu.

Jicho linayo mawea, majijicho yana mawi,
Lapenda kuchungulia, kuadhibu ja uchawi,
Jicho litazuilia, ‘pate’ milele uhawi.

Dua yangu kwako Mungu, nitibie jicho langu,
Moyo yaishe machungu, ‘sihangike’ ja kulungu,
Nitunzie jicho langu, nisitiwe kamwe pingu.

Mwangi wa Githinji
(Malenga wa mchanga Kati)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *