Una Nini Tu?

Mja wewe una nini, wadhani wewe ni nani?
Tangu pale hujioni, uonayo huamini?
Kipi hasa ni kiini, kutanuka kifuani?
Nakuasa ithamini, hadhi yako maishani.

Matoni pa Mkawini, sie sote vyombo duni,
Leo mbona watamani, ukajikweza juani,
Wengine kituonani, samadi barasteni?
Nakuasa ithamini, hadhi yako maishani.

Ukishaekwa enzini, watubana tulo chini,
Hutuoni masikini, twakanyagwa ja majani,
Duduvule sikizani, taungulia jitini,
Nakuasa ithamini, hadhi yako maishani.

¬© Okelo w’Esonga
Malenga Mtafunamiwa

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *