Tunda Tamu

Tunda lililo utamu, pachipachi likuapo,
Tunda linipalo hamu, kila kutwa nililapo,
Tunda linipalo jemu, mi nilitengenezapo,
Tunda langu la muhimu, hilo ladha nipatapo,
Tunda langu tunda tamu, hilo nilitafunapo.

Tunda hilo lilo sumu, mara nyingi upatapo,
Tunda lililo hukumu, ubichi ulitundapo,
Tunda hilo silaumu, popote nilionapo,
Tunda ni tunda adhimu, pale pote likuapo,
Tunda langu tunda tamu, hilo nilitafunapo.

© Kimani wa Mbogo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *