Chako Kijiko

Alonipa yerabuka, shukrani na’patia,
Babu yangu losifika, ‘fahamu lozidia,
Ujanani kakumbuka, mithali losimulia,
Hicho chako kijiko, sikwagure koko nacho.

Alotabiri rohoni, waziwazi twalola,
Vijanaa kama nyani, tamba kwa Motorola,
Wanawali nao nyuni, tafuta zo bakola,
Hicho chako kijiko, sikwagure koko nacho.

Mitaani kote wakera, wajomba na wavyele,
Utadhani ni wakora, kuwanasa mawele,
Macho yao yalengera, wala ‘looza mchele,
Hicho chako kijiko, sikwagure koko nacho.

Nafika mie kikomo, kupuliza kipenga,
Acheni wenu mgomo, wasikize wahenga,
Epuka raha za ngomo, makali yake ‘panga,
Hicho chako kijiko, sikwagure koko nacho.

© Kiambi Daniel
Mombasa, Kenya

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *