Dunia Maisha Suluhu

Ni ufalme wa Juha, kuzaliwa kwa mzaha,
Na kuishi kwa madaha, kulalama na kuhaha,
Ambulio ni jeraha, lenye kovu la karaha,
Kuishi siyo furaha, bali pambano za raha.

Kwa ndoido za barehe, na kungwi zake uhehe,
Zinakinai kwa kohe, waziishio mashehe,
Kuziimba zote duhe, ni lalamo za wasohe,
Maisha yao wahehe, dunia kwao kobohe.

Maisha ndiyo sahihi, kipimo cha wenye sihi,
Waendao kwa kubahi, ng’atuo zao jerahi,
Wabakio kwa kusihi, matunda yao kubuhi,
Dunia ni mmasahi, mawindoni yu sahihi.

Kubwakubwa kama hoho, rangi kijani ya koho,
Pepesuko la kijiho, tipwatipwa kama boho,
Amani yake kiroho, yenda mwendo wa kohoho,
Dunia haina roho, maisha kuyapa hoho.

Jaribio za kubuhu, kwa kutafuta suluhu,
Pasi kuleta ujuhu, wenye mwendo wa baruhu,
Najinyima kimya pwahu, kwa dalili za huhuhu,
Maisha yote maduhu, dunia mwendo kiduhu.

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *