Simba Chuchule

Simba chuchule atamba, mla mamba kujigamba,
Matapishi kuyalamba, juu ya mgumu mwamba,
Abishana naye nge, kupepea kama tunge.

Simba mbio zake timba, maishaye si membamba,
Sauti safiri gumba, zorote juu ya kamba,
Simba huyu ndiye singe, jicho mithili ya mwenge.

Akuwinda kwa taramba, udelele kuuramba,
Alangua juu ya shamba, arukaruka kwa tamba,
Abishana naye nge, kupepea kama tunge.

Simba azalisha mende, simba huyu hula tende,
Alemewa na matinde, jicho pua aliponde,
Simba huyu ndiye singe, jicho mithili ya mwenge.

Njaa humfanya mwende, asikilize sikinde,
Unga usage uponde, simba akwepa upinde,
Abishana naye nge, kupepea kama tunge.

Simba rafiki wa kenge, mamba kuwa naye tenge,
Simba varishwa kitenge, pori ingia mkenge,
Simba huyu ndiye singe, jicho mithili ya mwenge.

Mnyooko niupinde, muinamo niupande,
Kesho yao waipange, kwa muwindo wa ugange,
Abishana naye nge, kupepea kama tunge.

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *