Imani Yetu Imara

Nanga ninang’oa sasa, natunga kuwaaseni,
Kwa furaha na bashasha, wanayosefu kamili,
Mengi ndugu tawapasha, tushukuru mola kweli,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Kanisa nyumba ya bwana, na ndio yetu makao,
Yetu mambi kwa rabana, hayo kwetu huwa ngao,
Mungu baba naye Mwana, Roho kwetu mazao,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Kanisa si lazi jumba, yetu mwiyo ni sanika,
Sala zetu kwa muumba, kwetu iwe ni baraka,
Twasadiki tukiimba, furaha kwake rabuka,
Imani yetu imara, nasi baraka nazo teletele.

Sakramenti zote saba, ubatizo nanga take,
Ekaristia si haiba, wenye ndoa watukuke,
Padrisho paroko baba, wagonjwa uwapake,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Kitubio sakramenti kuu, dhambi zetu tuoshe,
Mwili damu yake kuu, kipaimara twajizolea,
Kitekizimu somo kuu, ukweli tuagundua,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Uongozi kanisa bora, Mtakatifu Baba Roma,
Moyoni Nina naima, tena isothimilika,
Sala lojaa neema, kwake baba Rabuka,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Ni muhimu sangilia, mola ametujalia,
Kadinali askofu pia, kwa mwenyezi metumikia,
Padre, watawa seminaria, kwake tunafurahia,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele,

Baba yetu wa mbinguni, Sala alotufunza Isa,
Alijitoa msalabani, kwa yake Mola ruhusa,
Twamwabu altareni, mienendo yetu tasahihisa,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Kila kitu itakoma, Siku hiyo ikifika,
Siku hiyo tasimama, mbele ya Baba Rabuka,
Kitubio pokea Sana, dhambi taziepuka,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Nikafanya uchopezi, nikiwa sugu kibaka,
Msalaba twika njiani, machozi yanitiririka,
Pasaka sherehe kanisani, mkombozi kafufuka,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele,

Nyuso zetu twainamisha, altare tupe heshima,
Moja kwetu ni kanisa, takatifu misa hima,
Vyema kanisa rembesha, yetu imani wima simama,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Rosari twasali siku kila, Mama maria heshima jaza,
Oktoba mwezi nyingi sala, neema za kristu sitapeza,
Litania watakatifu kwetu ala, mbinguni sala fululiza,
Imani yetu imara, Baraka nazo teletele.

Beti tatu kumi twamaliza, kwetu si himizo nasi,
Dhambi tena sitasaza, mema hizi nizihisi,
Katoliki imani tunza, kwa mola ndilo kasisi,
Tulitunze imani yetu, Nasi Baraka tujazwe.

© Br. Koffi Brian

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *