Neno la Adabu

Jambo uombapo, tafadhali sema,
Lako liwe lipo, laonyesha wema,
Kitu uombapo, omba kwa heshima,
Neno la adabu!

Sema samahani, pale ukosapo,
Uombe idhini, uzungumzapo,
Mwambie fulani, heshima iwepo,
Neno la adabu!

Kumradhi sema, utendapo kosa,
Uwe mtu mwema, wa heshima hasa,
takuwa salama, mzuri kabisa,
Neno la adabu!

Yeyote alie, huyo kwa kuwaza,
Pole umwambie, mtu kuliwaza,
Wema umjie, baya kumaliza,
Neno la adabu!

Maombolezini, mwambie makiwa,
Umpe moyoni, neno kuambiwa,
hivyo si utani, mtu akifiwa,
Neno la adabu!

Asante mwambie, neno shukrani,
Wema umwingie, fikira wazoni,
Mema mfantie, kwonyesha wazoni,
Neno la adabu!

© Kimani wa Mbogo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *