Ukweli

Nawaeleza ubayana
Myajue ya jana
Tuzidi kusikizana
Yangu nileta manena

Yangu nilileta manna
Ukweli kusemezana
Tusked kudanganyana
Kuwa ‘siku ni mchana

Kuwa ‘siku ni mchana.
Ni uongo si bayana
Wacha uambie maana
Usio u’ngo kujikana

Usio u’ngo kujikana
Uwezii kujibana
Ukifikiri kwa kina
Ya uongo kujikana

Ya uongo kujikana
Ikiwa ni ubayana
Tuzidii kula shan a
Kwetu yawe ya kufana

Kwetu yawe ya kufana
Wala si ya kite ng an a
Tusemapo kukutana
Yetu mambo faraghana

Yetu mambo faraghana
Yasiwe kuudhiana
Kwetu bali we fakana
Usio kuchukizana

Usio kuchukizana
Wala uwe kupendana
Letao matangamana
Bila sisi kukatana

Bila sisi kukatana
Wino wangu nauchuna
Tusiwe wa kuyabana
Moyoni kuumiana

© Vincent Okwetso
Malenga wa Butula

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *