Kifo Takushitaki

Kifoo nakulizaa, mbona huna hurumaa,
Watu wengi mechukua,lini utatoshekaa,
Kiwewe umenitia, mwaka gani taridhikaa,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Zangu rafiki ‘chukua,huku nahuzunikaa.
Ma’zoni meningizaa, fikirani menitia,
Mauti we wamizaa, mashakani watutia,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Nani aliyekuzaa, niwezee kumjua,
Ukweli kuelezwaa, nijue ubayanaa,
Hakika unasinyaa, kwa yote natutendaa,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Bibi yangu lichukua, hata babu kamezaa,
Lini we taridhikaa, nasi ‘we bila udhia,
Siku ipi takomaa, nasi tuweze pumua,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Dada yangu kachukua, kitendo ukakanaa,
Moyoni nikadhikaa, mawazo kanizongaa,
Upweke kaniwachia, mbi afya nikapataa,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Na kaburi mwafanaa, kila siku mwa’tanaa,
Lini mtatenganaa, nasi tu’pumzikaa,
Wapenda kututengaa,Pasi kuu malezaa,
Kifoo takushitaki unieleze ukweli.

We umetupokonyaa, wetu nchini mashujaa,
Satoti umemlaa, bila we kuridhikaa,
Nkaiseri ka’ndoshaa, pasi nasi fahamia,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Babangu kaondoshaa, na kaburi kumezaa,
Mashaka kanijazia, bila mulezi mwemaa,
Masumbuko mekuwa, tangu wangu uzawaa,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Msando ukamwibaa, mafaa ukaletaa,
Chuki ikaeneyaa, yako ma’ko sabubaa,
Uoga ukaingia, ndani nyumba jifungia,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Rasi mosi kamezaa, mwanzilishi wa tafaa,
Maathai naye pia,’penzi wa mazingiraa,
Nani umetuachia, kigogo wa taifaa,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Changu kikomo natia, wako kweli nangojaa,
Nifahamu yako nia,tupate kutoshekaa,
Mauti we wasumbua, watu sio na dowaa,
Kifoo takushitaki, unieleze ukweli.

Vincent Okwetso
Malenga wa Butula.

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *