Swala Kwangu Utamaduni

Jumapili narauka, yangu rosari shingoni
Zangu njia ninashika, kwelekea kanisani
Malangoni nikifka, nandaa yalo moyoni
Sala popote nilipo, wa kwangu tamaduni

Mahubiri yaniingie, nafsini nikajishaue
Utu wema niuwazie, ubaya unepukie
Mia zaka nijitolee, kwa mwenyezi zimfikie
Sala popote nilipo, wa kwangu utamaduni

Namshukuru Rabuka, kwake nasema dayani
Moyoni nakiri hakika, nisije lowa hayawani
Kwa sauti nasikika, nakemea ya gizani
Sala popote nilipo, wa kwangu utamaduni.

Kwake mola nitulize, tamati niafikie
Sala zangu inilize, beti nne nishukie
Kusudi nitimize, jasadi langu lizimie
Sala popote nilipo, wa kwangu utamaduni.

© Koffi Brian

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *