Ukufunzi Sio Njuga Yako

Salamu pokea kaka,Ewe ulo mtaani,
Kuning’oa ulitaka, nimehamia mjini,
Kwangu ‘meleta baraka, najua hutaamini,
Ukufunzi vua bwana,sio njuga yako katu.

Kikomo mtu hafiki, kazini akifutwa,
Umilisi unabaki, kwingine anaitwa,
Akipa kisogo dhiki, shwari tele kujaliwa,
Ukufunzi vua bwana,sio njuga yako katu.

Kama kupe umenata, chuo hicho hung’atuki,
Umilisi huna hata, mtaala kumiliki,
Kazi yako hujapata, hiyo haikuafiki,
Ukufunzi vua bwana,sio njuga yako katu.

‘Taisha kuwa kabeji, shambani ukizoea,
Tafuta chako kipaji,ndugu acha kuzembea,
‘Sijifanye mjuaji, kwa kozi hukusomea,
Ukufunzi vua bwana,sio njuga yako katu.

© Lawrence Gaya
Malenga Chipukizi

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *