Siku Hii Siku Yako

Kwa jasiri najitosa, simulie yamoyoni,
Sitajuta kwa kosa, ya kimya kusema,
Wewe wangu kipusa, rohoni mesimama,
Hepi besdei mpenzi, siku hii Siku yako.

Wazidi jaza hamasa, wakati unapopita,
Moyoni nimenasa, siwezi jipepeta,
Wengi mewakosa, kwako wewe nimepata,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Siku hiyo nakumbuka, moja mwaka umepita,
Ukisali kwa rabuka, koo safi ukiita,
Moyoni lishtuka, sikutaka kukuhata,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Sala kwisha nikaita, ujasiri kanitoka,
Nilipatwa na utata, kutizama malaika,
Tamaa nikapata, ulipoaste hakika,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Miezi mepitia, machoni hukunipotea,
Uchao najipa nia, siku moja kuambia,
Kutani najigongea, nilipo kufukuzia,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Mekuwa kisubiria, siku nitapokwambia,
La moyoni kutoa, aibu sitajionea,
Machoni najililia, la asha menijibia,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Jawabu nijaza donda, nafsini niondosha,
Tafakari bila konda, mwenzio meniosha,
Mawazo nimekonda, juma sasa zimekwisha,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Mapenzi si lazi jumba, rafiki tutasalia,
Uchungu itanikumba, kwa kimya tajililia,
Fikra enda sambamba, tisti tasimamia,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Shukrani kwa wazazi, malkia menizalia,
Ya Leo siku na mwezi, mpenzi- rafiki nizalia,
Uwezo wake mwenyezi, taendelea kulea,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Ningependa kukuenzi, kwa kukupa hii dunia,
Ila hilo siliwezi, ndugu yangu katangulia,
Takupa lake penzi, furaha nawatakia,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

Koffi mie namaliza, melowesha ya moyoni,
Zidi kuniliwaza, mapenzi tele mpatie,
Ahadi mi nakujaza, maishani ufurahie,
Hepi besdei mpenzi, siku hii siku yako.

© Koffi Brian

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *