Yanyosheni Mapito

Na hiki changu kipenga, leo hii nakipuliza,
Niwalete kwenye mwanga, tembeao kwenye kiza,
Ninyi siwachi makanga, habari hii natangaza,
Yanyosheni mapito yenu, unyakuzi mewadia.

Kristu Yesu awapenda, ufunuo wake Mungu,
Yako nafsi tailinda, kivielewa vifungu,
Heshimako itapanda, na kuishi ya kiungu,
Yanyosheni mapito yenu, unyakuzi mewadia.

Limwenguni kwenu raha, tageuka kuwa balaa,
Fuatisha ya duniha, na kuishi kwenya gizaa,
Katiwa giza zeniha, ya ulimwengu kila wasaa,
Yanyosheni mapito yenu, unyakuzi mewadia.

Wakubwa wadogo pia, bahari dhambi wazama,
Shetani wakimbilia, potovuni watanzama,
Wahubiri simulia, geukeni mwesalama,
Yanyosheni mapito yenu, unyakuzi mewadia.

Tamati nimefikia, ya kiyama yaja siku,
Kwake Yesu kimbilia, taepuka na utungu,
Usiku nakaribia, nayuwaja mawinguni,
Yanyosheni mapito yenu, unyakuzi mewadia.

© Kiambi Daniel
Mombasa Kenya

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *