Ghala

Ghala linasikitika, kwa kulibwagia zani
Ghala linahuzunika, mekimbiwa na mizani
Ghala damu yachemka, lini tatoka gizani
Ghala kutwa mashakani, mashaka mengi mashaka.

Ghala lafahamu fika, lafa na tai shingoni
Ghala nuru yafifika, mengi mejaa pomoni
Ghala asema yafika, asubuhi na jioni
Ghala kutwa mashakani, mashaka mengi mashaka.

Ghala halina dhihaka, linasaka ahueni
Ghala linadhoofika, hima hima lioneni
Ghala roho inatoka, hewa chafu halineni
Ghala kutwa mashakani, mashaka mengi mashaka.

© Evock Miwaga

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *