Amezaliwa

Imanweli jina lake,
Aliacha enzi yake,
Hadi kuzaliwa kwake,
Na bikira mwanamke,
Mariam jina lake,
Josefu ni baba yake,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Adamu alipoumbwa,
Sheria aliwekewa,
Vyote kula ni salama,
La! Katikati ni homa,
Mema pia na mabaya,
Ujuzi kamuwekea,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Adamu kavumilia,
Sheria kuzingatia,
Tunda lile hakulila,
Eva mkewe akala,
Kwa kupenda kalileta,
Mumewe naye akala,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Adamu alipoasi,
Upweke ulitawala,
Hakuwepo Mungu nasi,
Adamu walijificha,
Nyoka ndiye ibilisi,
Uasi kawafundisha,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Aliujenga ukuta,
Mapanga ya makerubi,
Moto ukaizunguka,
Njia ile uzimani,
Hawakuweza kuruka,
Walibeba zao dhambi,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Huruma ni sifa yake,
Mungu aliye mbinguni,
Nani aje nimtume,
Akafike duniani,
Uhai wake atoe,
Awatoe utumwani,
Wanangu awakomboe,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Ishirini nne wazee,
Hawakupea salaba,
Wenye uhai wanne,
Walishindwa kuinuka,
Katokea mwanaume,
Kasema mimi naenda,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Ikafanyika mipango,
Mikakati ikawekwa,
Haikupita kitambo,
Tumboni akaingia,
Dhoruba zote kibao,
Kapita kujionea,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Tisa ilipohitimu,
Horini alifikia,
Watu wakapiga mbiu,
Mwokozi amezaliwa,
Tayari kwa majukumu,
Dunia kuifikia,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Nyimbo nazo ziliimbwa,
Amezaliwa mfalme,
Simba kabila la Yuda,
Kazaliwa mwanaume,
Mzuri kwa tawala,
Hekima anazo tele,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA.

Kuzaliwa kwa mwokozi,
Siyo upike pilau ,
Rojo minofu na ndizi,
Ufanye na siku kuku,
Moyoni mpe nafasi,
Dhambi zako uzitubu,
YESU NI KAKA MKUBWA
KAZALIWA KUTUPONYA

Kaka mkubwa ni Yesu,
Mungu kwetu ndiye baba,
Ukimwomba anajibu,
Usipokata tamaa,
Uliyekosa utubu,
Katangaza msamaha,
YESU NI KAKA MKUBWA
YESU NI KAKA MKUBWA!

© Elijah Meshack

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *