Mwanafunzi Tia Ari

Ulingoni najitoma, ya moyoni nieleze
Nisibaki na lalama, kwa kalamu nimalize
Asilani sitokoma, na tamaa sikatize
Tamaa usiikate, siku njema itafika.

Darasani ukifika, makinika ufahamu
Rafikizo wakichoka, kuimudu na elimu
Tamaa ishawatoka, wakabaki bila hamu
Kuvua maji ya kina, kwataka mtaalamu

Na nidhamu udumishe, ni muhimu maishani
Daima jibidiishe, usilale darasani
Yalopita tuyapishe, tuyalenge ya usoni
Likiwika lisiwike, kutakucha mwanagenzi.

Kaditama nimefika, dukuduku limetoka
Mtihani ukifika, sije kasisimka
Usikose makinika, Hilo Nimesha litamka
Siku moja itafika, bila Shaka siku njema

Bwana Wamui Paul

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *