Onesha Onesha!

Rijali rijali, tenda ya rijali,
Kubali kubali, acha ubatili,
Aili aili, kuacha kubali,
Onesha onesha, wako urijali!

Kasisi kasisi, tenda ya kasisi,
Kiasi Kiasi, nenda e’ Kasisi,
Sighasi sighasi, nenda Tarisisi,
Onesha onesha, wako ukasisi!

Jasiri jasiri, tenda ya jasiri,
Tayari tayari, sifanye ya siri,
La heri la heri, twone yako heri,
Onesha onesha, wako ujasiri!

Jasusi jasusi, tenda ya mwalimu,
Nidhamu nidhamu, tuone hudumu,
Haramu haramu, iwapo hujumu,
Tuonyeshe, wako ualimu!

Rasisi rasisi, tenda ya raisi,
Waasi waasi, fanya ugumu kesi,
Rahisi rahisi, waende waasi,
Onesha onesha, wako uraisi!

Chakari chakari, tenda ya chakari,
Subiri subiri, sikubali shari,
Chichimiri chichiri, hiyo chichimiri,
Onesha onesha, wako uchakari!

© Kimani wa Mbogo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *