Nitongoze kwa Mpango

Dada umeshapanuka, maadili kutanduwa,
Asili umegeuka, mila za kufatiliwa,
Sitoweza shawishika, dada hujanitambuwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!

Wabisha wangu mlango, chumba changu wakijuwa,
Uwazi wako mgongo, wanionesha maziwa,
Kumbe unayo malengo, wanijia kusumbuwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!

Tabasamu sihitaji, mezoea kutendewa,
Unialikapo siji, tabiazo nazijuwa,
Sijibu ukinihoji, sipendi kusailiwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!

Usiku ati hulali, kwa mawazo umejawa,
Bila kuniona huli, nijapo hamu ukawa,
Wadai legevu mwili, ukadhaniwauguwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!

Litakufika la mori, ujapo katimuliwa,
Dadangu ungesubiri, mtazamokuambiwa,
Ya wawilisio siri, hadharaninatumbuwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!

Kamtafute mwengine, mjinga na wa kuliwa,
Mabozi mkabwiane, mahaba mkajaliwa,
Ovu lazima ninene, niweze kujinasuwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!

Sijaola wanawake, hawatendihutendewa,
Ngoja ukatawalike, waumekukutambuwa,
Heri leo uudhike, ukweli ukaujuwa,
Nitongoze kwa mpango, kila mwendo ni hatuwa!

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Your email address will not be published. Required fields are marked *