Aina/Bahari Nyinginezo

  1. Kimai ni aina ya tungo zinazozungumzia shughuli za uvuvi na maisha ya baharini.
  2. Zivindo ni mkondo wa shairi unaojengwa kwa maana mbalimbali za maneno kutolewa. Hupatikana sana kwa ushairi wa jadi.
  3. Wawe/wave ni tungo za kishairi zinazozungumzia masuala ya ukulima.
  4. Dura mandhuma/inkishafi ni tungo za kishairi ambazo aghalabu huwa na mizani kumi na moja kila mshororo na zina bahari kama tenzi. Kipande cha kwanza huzua hoja au swali ambalo hukamilishwa na sehemu ya pili.
  5. Ushairi wa kiabjadi ni ushairi ambapo kila herufi ya kwanza ya mshororo maalum katika ubeti hufuata mpangilio wa kialfabeti au kiabjadi.
  6. Ushairi ruwaza ni ushairi ambao huchukua muundo au sura ya kitu fulani kinachozungumziwa. Pia huitwa ushairi maumbo.
  7. Utendi ni aina ya utenzi unaizungumzia maisha na matendo ya shujaa/mashujaa wa jamii fulani, mapisi ya mahala, wasia au maudhui mengine yanayoendelezwa kwa urefu.
  8. Zingo ni aina ya mkondo wa shairi ambapo neno la mwisho la mshororo huanzia mshororo unaofuatia na ubeti unaofuata.