Uhuru wa Mshairi

Mshairi amekubaliwa kutumia lugha namna anavyotaka wakati anatunga shairi. Anaweza kukiuka kanuni ambazo hutawala sarufi. Uhuru huu humsaidia kukidhi mahitaji ya kiarudhi kama vile urari wa vina na usawa wa mizani.