Mandhari Yapendeza. Ni shairi la msuko linaloisifia mandhari na kumsifu Mungu kwa kuipamba. Mandhari Yapendeza


Mandhari Yapendeza

Mandhari tulopewa, ni bora na mahsusi,
Sifa zake maridhawa, tujivunie halisi,
Mara tupungapo hewa, twauona ufalisi,
Mandhari yapendeza.

Machweo niamkapo, husikia zao nyuni,
Nyimbo wazienezapo, mandhari wakighani,
Hizo nipatilizapo, wakamsifu angani,
Mandhari yapendeza.

Jua hutuangazia, daima hujitokeza,
Angani laning’inia, nao mwanga kuangaza,
Mandhari angazia, na daima kupendeza,
Mandhari yapendeza.

Dunia yeye karemba, mithili ya kurembeka,
Nayo mbingu kaipamba, kiwango cha kupambika,
Kukwatua kwa kupamba, na bahari kukwatuka,
Mandhari yapendeza.

Kitaru cha utulivu, kisicho nacho kivumbi,
Noana maji maangavu, wanamaji yao kambi,
Samawati na kijivu, ilazimishayo fumbi,
Mandhari yapendeza.

Kunyaa ni leo peke, gimba likuwapo kali,
Keshoye yasinyuuke, yatakuwepo jamali,
Ndo nasema atukuke, Mola aliye jabali,
Mandhari yapendeza.

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

*