Kipindi Cha Nne

(Wanamapinduzi na Wanamapokeo)

Katika kipindi hiki, kulizuka wasomi wenye ujuzi katika Fasihi ya Kiswahili. Wasomi hao walijiita Wanamapinduzi. Walijitokeza na aina ya mashairi yanayojulikana kama Mashairi Huru na kudai kuwa yanakubalika katika kama mashairi mengineyo.
Wanamapinduzi hao walisitiza kuwa mashairi ya arudhi yalimfunga sana mshairi kupasha ujumbe wake vizuri. Walidai kuwa mshairi hakuweza kujieleza vizuri kwa kuwa ilikuwa ni lazima ajibiidishe kwanza kutafuta maneno yatakayolinganisha vina na kutosheleza mizani. Waliamini kuwa mtunzi ana uhuru wa kutunga aina za mashairi wazipendazo bora tu wapashe ujumbe kwa hadhira. Washairi hao walitunga mashairi bila kujali arudhi za ushairi, jambo ambalo lilizua mgogoro katika Ushairi wa Kiswahili.
Baadhi ya watunzi hao ni kama:

  • Euphase Kezilahabi
  • Mugyabuso Mulokozi
  • Ebrahim Hussein
  • Alamin Mazrui
  • Kithaka wa Mberia
  • Kulikoyela Kahigi