Kipindi Cha Kwanza

(Urasimi Mkongwe)

Kipindi hiki ni wakati wa mashairi yaliyotungwa kabla ya karne ya kumi na nane. Katika kipindi hiki, mashairi yalikuwa kakitungwa ila hayakuwa na utaratibu wa vina, vina, mizani na beti kama ilivyo katika mashairi ya kisasa. Mashairi ya siku hizo yalikuwa kama nyimbo tu na yalikuwa na mishororo mirefu. Mashairi hayo yalibadilika kimaudhui, jamii nazo zikipambana kutunga kwa maudhui mbalimbali.

Mashairi ya myakazi hizo, yalipashwa tu wakati wa sherehe mbalimbali kwa kuwa ustaarabu wa kuandika ulikuwa bado kwa Waswahili. Mabadiliko mengi yalifanyika Waarabu walipofika pwani ya Afrika Mashariki. Waarabu walikuwa na mashairi yao yaliyokuwa na vina beti, mizani na maudhui ya kidini (dini ya Kiislamu). Tangu wakati huo, mashairi yakfuata mkondo huo. Waswahili wakafunzwa hati ya Kiarabu ili kusoma Kurani Tukufu.

Hizo ndizo nyakati ambazo inadhaniwa kuwa shairi la kwanza liliandikwa kwa kufuata kanuni za Ushairi. Japo kulikuwa na mashairi mengine hapo awali, Utenzi wa Tambuka (Chuo cha Herekali) unadaiwa kuwa wa kwanza kuandikwa kwa kufuata kanuni za Ushairi. Utenzi huo ulitungwa na Mwengo Bin Athumani (1728-1840) na ulihusu maisha ya Sultani wa Pate ‘Fumo Laiti Nabhani’.

Tungo nyingine za wakati huo:

  • Utenzi wa Hamziya (1749) – Sayyid Abdarus
  • Utenzi wa Mwanakupona (1859)
  • Utenzi wa Al-Inkishafi (1813) – Sayyid Abdallah A. Nassir
  • Utenzi wa Rasi-al-Ghuli
  • Utenzi wa Shufaka
  • Tungo za Muyaka bin Haji Al Ghassany (1776-1840)
  • Tungo za Ali Kofi
  • Tungo za Bwana Mataka