Uainishaji Kuzingatia Wahusika

1. Ngonjera

Ngonjera ni shairi lenye wahusika wawili wanaojibizana. Kwa mfano; Mwalimu na mwanafunzi, mzazi na mtoto, nk.
Mfano:

MWANA:

Babangu ninalo swali, kwa kweli lanisakama, 
Jicho unalo fahali, sitakwambia tazama,
Swali langu la fasili, hatupati hali njema,
Nieleze nielezwe, mbona tukose baraka?

BABA:       
 
Ili upate baraka, kwa wazazi fanya vyema,
Hali njema ukitaka, mwena uwe na heshima,
Wazazi, dada na kaka, kwao iwe taadhima,
Mwanangu tega sikio, na heshima iwe ada.