Kipindi Cha Tatu

(Urasmi Mpya)

Kipindi hiki kilikuwa kati ya 1945 na 1960. Washairi walitunga kwa kufuata kanuni za ushairi. Wengi wa watunzi hao walitunga mashairi ya tarbia ingawa wengine kama Shaana Roberts walitunga aina tofauti ya mashairi. Kipindi hiki kilikuwa cha Wanajadi au Wanamapokeo walishindania ufundi. Ilikuwa ni lazima kila mtunzi kutumia arudhi za ushairi ili kuonyesha kuwa, alikuwa bora kuliko mwengine. Shairi ambalo halikufuata kanuni hizo, halikuaminika kama shairi kamili na liliitwa guni. Waliamini kuwa shairi ni lazima liwe urari wa vina na ulingasnifu wa mizani.
Tamasha mbalimbali ziliandaliwa na watunzi kuwasilisha tungo zao na kufanyiwa uamuzi na watunzi waliobobea wakajulikana kama mashekhe. Waliofaulu walivikwa umalenga nawaliopungukiwa katika arudhi yoyote kubezwa na kuvikwa guni.
Watunzi waliosifika sana wakati huo walikuwa kama:

  • Mwengo Bin Athumani
  • Muyaka bin Haji
  • Mwalimu Sikujua
  • Said Karama
  • Amri Abedi
  • Ahmad Nassir
  • Shaaban Robert

Umaarufu wa washairi wa kipindi hiki ulidhihirika wakati wa tamasha mbalimbali na sherehe kama za arusi, mazishi na burudani. Tamasha hizo zilisaidia kunoa na kuboresha vipawa vyao.