Uainishaji Kuzingatia Mandhari

1. Wajiwaji/Takhmisa

Tungo hizi zilitokana na tungo za takhamisa ya Kiarabu inayoitwa Madihi yenye maudhui ya dini. Mashairi ya aina hii yalikuwa na mishororo mitano kwa kila ubeti. Kila mshororo ulikuwa na mizani 15 na ulikuwa kipande kimoja tu. Mashairi haya zamani yalitungwa na watu wawili, mshairi mmoja akitunga mishororo mitatu ya kwanza ya ubeti na mwenzake akitunga mishororo mingine miwili ya mwisho kwa kila ubeti bila kuharibu maana ya shairi lenyewe. Mfano wa wajiwaji unaojulikana sana ni ule wa Sayyid Abdalla Ali Bin Nasir uliohusu Shujaa Liyongo:

Anami shujaa samba ndole mwondoa ari
Mvunda kilaa na husuni kizidabiri
Nayipija kifa kayitia katika shari
Sichi mata yao na mafumo yanganawiri
Mandi mafuamati na magao mauya nyuma.

2. Hamziya

Bahari hii ilipata jina lake kutokana na Kasida ya Hamziya ambao ni utenzi wa Kiarabu. Utenzi huo uliandikwa karne ya 13 na mshairi wa Misri aliyejulikana kama Al-Busiri kwa lengo la kumsifu Mtume Muhamad. Kasida ya Hamziya ilitafsirirwa kutoka kwa Kiarabu na Sayyid Aidarus bin aliyezaliwa. Tazama baadhi ya beti zake:

Amani, amani hakika wo mtima wangu
Kwa dhambi tendazo ni mtovu kwako fahama.

Niisikemiye kwa pendezo nyingi ambayo
Wanishikimiye shufaau nayo iswima.

Mulungu waiza kupatami viwi bihali
Na miye wagamio kwako imama.

Twakutumaile kwayo mambo ambayo kwamba
Baridi iyapo mitimani ningajahima.

Tujile uliko tuziliwo na ufukara
Ututukuliya ukwasiwo dhaifu nyama   
Kasida ya hamziya wahitaji ilikuwa na mishororo miwili miwili iliyokuwa na kipande kimoja tu. Kina cha kwanza kwa kila mshororo kilikuwa si lazima kiwe sawa na cha mshororo wa pili lakini vina vyote vya mshororo wa mwisho vilikuwa ni lazima viwe na urari.

3. Utumbuizo

Utumbuizo ni shairi lililoimbwa kwa lengo la kutumbuiza, kuchangamsha au kufurahisha. Tumbuizo zilikuwepo hata kabla ya kuja kwa Waarabu. Kwa sasa, tumbuizo si maarufu sana kwa sababu ya nyimbo. Huwa na idadi kamili ya mishororo na mizani, urefu wa mshororo hutegemea pumzi aliyo nayo mwimbaji na lengo lake.

Huwa zina vina vya mwisho lakini zipo zenye vina vya kati, bila mpangilio maalum.

Mfano mwema ni Utumbuizo wa Mwana Nazi wa Fumo Liyongo alioelezea sifa za mke mzuri. Tazama baadhi ya beti zake:

Kamba twende tangulia naya,
Kamtuze aate simazi,
Kamwandama nyuma kiyongoya,
Akinuka miski na mbazi.

Akangia kamupa salamu,
Kamjibu mwana wa hijazi,
Saa hiyo kondoka akema,
Kamwandikia mkono wa fuzi.