Bahari Nyinginezo

Msemele/Kifunga Nyama

Msemele ni shairi ambalo mtunzi hutumia lugha iliyojaa ufundi mwingi kama tamathali nyingi za usemi, methali na maneno ya hekima.

Ushairi wa Kiambo

Hii ni aina ya ushairi ambapo tungo inahusu kitu na mazingira yake kama vile mji, mlima au mto.

Kasida/Qasida

Kasida ni tungo zenye maudhui ya kidini. Hutumiwa kumsifu mtu au jambo fulani. Kasida pia huimbwa na Waislamu kumsifu Mtume Muhammad katika Maulidi, sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad.

Kimai

Kimai ni aina ya tungo zinazozungumzia shughuli za uvuvi na maisha ya baharini.

Wawe/Wave

Wawe ni tungo za kishairi zinazozungumzia masuala ya ukulima.

Ushairi wa Kiabjadi

Huu ni ushairi ambapo kila herufi ya kwanza ya mshororo maalum katika ubeti hufuata mpangilio wa kialfabeti au kiabjadi.

Ushairi wa Ruwaza

Ushairi wa ruwaza ni ushairi ambao huchukua muundo au sura ya kitu fulani kinachozungumziwa. Pia huitwa ushairi maumbo.

Zingo

Zingo ni aina ya mkondo wa shairi ambapo neno la mwisho la mshororo huanzia mshororo unaofuatia na ubeti unaofuata.

Kumbukizi

Kumbukizi ni mashairi yanayoelezea kuhusu kumbukumbu ya matukio maalum kama ya kihistoria, shujaa au kidini.

Ushairi wa Ruwaza

Ushairi wa ruwaza ni ushairi ambao huchukua muundo au sura ya kitu fulani kinachozungumziwa. Pia huitwa ushairi maumbo.

Zohali

Zohali ni mashairi huru ya kisiasa yasiyozingatia arudhi za ushairi.

Tiyani Fatiha

Bahari hii ni ya ushairi wa kidini wa kuomba toba. 

Sama

Sama ni aina ya ushairi ambapo mshairi hutunga kwa kutumia mahadhi ya wimbo wowote wa zamani.

Kitwanga

Hizi ni nyimbo zilizoimbwa na Waswahili wakati wa kutwanga na kupepeta mpunga.

Mbolezi

Hizi ni nyimbo za kuomboleza wakati wa kifo. Ni nyimbo za huzuni na hutumika wakati wa matanga. Kabla ya kuja kwa Waarabu, Waswahili pia waliziita Tahalili.

Mashairi ya Ngano

Mashairi haya hutumiwa na mshairi ili kusimulia ngano. Mfano mzuri ni Hadithi ya Kitoto.

Mashairi ya Ukombozi

Mashairi ya ukombozi ni ya kutetea haki na uhuru ili jamii ijikomboe kutoka kwa utawala mbaya.