Kijacho Kinapokuja
Wapo baadhi ya watu wasiopendezwa na utu. Hutenda kinyume cha matakwa ya binadamu. Anapotenda, jamii humgeuka na kumtendea, kijasho kikamtoka. Litazame shairi hili… Kijacho Kinapokuja
Kitovu cha Ushairi, Washairi na Mashairi
Wapo baadhi ya watu wasiopendezwa na utu. Hutenda kinyume cha matakwa ya binadamu. Anapotenda, jamii humgeuka na kumtendea, kijasho kikamtoka. Litazame shairi hili… Kijacho Kinapokuja
Sijui kama unamfahamu vema jirani yako au mtu mnayeshirikiana naye kwa karibu mno. Na suala la “Nyumba Kumi” linapotajwa sijui linaibua hisia gani kwenye fikra zako. Baadhi ya watu tunaoishi pamoja, huenda wasikufae kwa chochote au lolote.
Wengine watakutumia, wakunongeshe na kukudhalilisha, hasara kwako. Wengine ni wanafiki wasio na utu, wasiokutendea lolote la hisani. Hata kama utamwamini aliye karibu nawe, usimtegemee wala ukadhani ni malaika kwako. Hili halimaanishi wewe usimtendee wema. Tenda wema nenda zako.
Shairi lifuatalo linaelezea kwa kina suala hili. Mhusika anahofia kwamba mtoto wake ataumwa na jibwa la jirani. Hili lalinganishwa na maovu anayoweza kufanyiwa na jirani yake. Ni shairi linaloonya kuhusu ushirikiano wako na jirani au mwandani wako wa karibu. Linamfahamisha hatari zinazomkabili kuwa na jirani asiye na matendo mema. Jibwa Litaniumia Toto
Watakusema na wakudharau lakini hayo hayatabadilisha maisha yako. Shairi hili linawashauri wenye tabia kama hizo kukoma na kushughulikia mambo yao binafsi. Lisome kwa makini. Nyumba Usiyoilala
Wanaopayuka huudhi mno. Watasema chochote bila kujali wala kuchunguza. Huwa ndio asili ya lolote linalosemwa bila kujali. “Kidomodomo waudhi, kupayuka kwanongesha!” Kupayuka Kwanongesha
Si jambo la busara kunidharau. Hujui kesho au hatima yangu. Usinidharau! Usinibeze! Usinidhulumu! Mbona Wanizaba Kofi