Uhakiki

(Pia huitwa Tahakiki, Uhariri au Tahariri)

Uhakiki ni uchambuzi wa maandishi yoyote, vitabu au majarida kwa kufafanua kwa kina tathmini yake kwa kukosoa na kusahihisha. Hili hufanyika kwa kudadisi mbinu zilizotumika, maudhui, lugha na ufasaha, ukweli na uwongo uliomo ndani ya maandishi. Maoni hutolewa baada ya kufanya uhakiki.