Mashairi yana umuhimu wa kipekee katika jamii kama ifuatavyo:
- Kuibua hisia za kuburudisha na kuhuzunisha
- Kukosoa, kukashifu na kubadilisha tabia zisizofaa katika jamii
- Kupasha ujumbe kwa hadhira kwa njia ya mvuto
- Kuelimisha, kuhamasisha na kuzindua jamii
- Kuhifadhi matukio muhimu ya historia ya jamii
- Kuhifadhi na Kuendeleza Utamaduni
- Kukuza Ushujaa, Ujasiri na Uzalendo
- Kufikirisha na kunoa fikra
- Kuliwaza
- Kuonya, kutahadharisha, kunasihi na kuelekeza
- Kuadilisha na Kuadibisha
- Kusifia mtu au kitu
- Kuendeleza na kukuza kipawa cha utunzi
- Kupamba, kukuza na kuineza lugha
- Kuhifadhi msamiati wa lugha ya Kiswahili na Sanaa ya fasihi
- Kuburudisha hadhira na wasomaji
- Kukejeli au kukemea mambo yanayoenda kinyume na maadili ya jamii
- Kuwasilisha hisia za ndani za mtu na mawazo