Zoezi la Kutunga

Tunga shairi la beti tano ukitumia maagizo yafuatayo. Iwapo utatunga shairi inavyofaa, utakuwa umehitimu masomo haya.

Maagizo

  • Shairi lenyewe liwe na maudhui ya suala la Heshima.
  • Dhamira iwe ni kuwasihi vijana wawe watu wenye heshima.
  • Liwe shairi la mtiririko kwa vina -MA (ukwapi) na -NI (utao).
  • Shairi liwe na kibwagizo na kichwa mwafaka.
  • Shairi liwe la beti tano, tarbia na mizani (8, 8) kwa kila mshororo.